Mambo 10 yanaweza kuwa kama kichocheo cha usaliti katika ndoa ambayo hasa ni tatizo la moyo
1. Kutokuvutia tena
• Moja ya sababu iliyopelekea kukubali kuoa au kuolewa na huyo mwenzi
wako, kuna baadhi ya vitu ulivutiwa navyo ndio akawaacha woote na
kumchagua huyo. • Vitu hivyo usipovizingatia na kuvi “maintain”
vitasababisha hali ya kukinai kwa mwenzi wako na mwisho kuanza kuvutiwa
na wengine kule nje.
2. Kutokujali tena kuwa unaongezeka unene,
kubadilika unavyoonekana na • Kila mwanandoa ana “test” yake ya mvuto
kwa mwenzi wake. • Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya wembamba wako
sasa unapojiachia na kuwa mnene ila hamu ya kuendelea kuvutiwa nawe
inapungua na baadaye inakwisha na kusababisha aanze kuchungulia nje ya
“fance” • Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya unene au kujazia katika
maeneo Fulani Fulani. Sasa mwili ukiporomoka unapoteza ule mvuto tena na
kumfanya apoteze hamu ya kuwa na wewe na kumfanya kuanza kuchungulia
chungulia nje. • Ni vizuri kujali afya yako na kujua ni vitu gani
vinavyomvutia mwenzi wako kutoka kwenye mwili wako na ujitahiti
kuvitunza “maintain” ili kuendelea kudumisha ule mvuto kwa mwenzi wako. •
Kumbuka kwamba tunaishi katika mwili. …
3. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.
• Tendo la ndoa ndio mhimili unaoishikilia ndoa. • Ukiona hamu ya tendo
la ndoa imepungua kwa mwenzi wako ujue majanga yanakunyemelea. •
Kufanya tendo la ndoa mara chache miongoni mwa wanandoa ni ufa wa
kubomoa ukuta na ulinzi wa ndoa. • Muda si mrefu utaanza kutamani
wengine na mwisho wake utaangukia huko.
4. Kukosa hamu katika mavazi mazuri kwa ujumla, mtindo wa nywele na jinsi unavyoonekana.
• Hili hasa ni kwa wanawake. Kable ya kuolewa ulikuwa unajitahidi sana
kujipamba na kujitunza kila wakati ulikuwa safi na nadhifu. • Pochi yako
ilikuwa haikosi vi pafyumu pafyumu. Sasa umesahau hata bei za pafyumu
zinauzwaje. • Sasa umeolewa, unashinda na upande wa kanga au kitenge
kifuani toka asubuhi mpaka jioni wala huna habari. • Mumeo kila
akikuangalia mpaka haamini kama ni wewe aliyekuoa ukiwa mrembo na wa
kuvutia. • Unavaa nguo nzuri tu pale tu unapotoka kwenda kanisani au
mtoko maalumu.
5. Kukosekana kwa mawasiliano • Mawasiliano yanaushisha pande zote mbili. • Anayetoa na anayepokea
6. Kushindwa kuendeleza yale yanayompendeza kila mmoja wenu. •
Mnakubaliana mipango kama wanandoa lakini utakelezaji unakua mgumu. •
Mmoja anakuwa tayari kutekeleza na mwingine anashindwa. • Aliyetayari
kutekeleza anavunjwa moya sana na Yule ambaye sio mtekelezaji
7. Ndoa za kipindi cha likizo.
• Wanandoa wanaonana siku kumi na nne tu kasha kila mtu anasafiri
kurudi anakofanya kazi. • Wapo baadhi ya wanandoa kutokana na mazingira
yao ya kazi wanaonana kila baada ya miezi 6 au wengine hata mara moja
kwa mwaka. • Hii hasa ni kwa wanandoa wanaofanya kazi mikoa mbali mabili
au nchi mbalimbali. • Wanatafuta pesa wakiua ndoa zao kwajili ya kusaka
pesa. • Ni heri kuacha kazi hiyo na kuishi maisha ya kawaida kuliko
kuwa na ndoa kama hii. • Kiufupi hii sio ndoa.
8. Kushindwa kushirikiana chumba cha kulala.
• Zipo baadhi ya ndoa mume analala chumba chake na mke analala chumba
chake. • Wapo wanandoa pia ambao wanalala chumba kimoja ila vitanda
tofauti • Kuna wengine wanalala chumba kimoja ila mmoja analala
kitandani na mwingine analala chini.
9. Kushindwa kumfikisha mwenza wako mara kwa mara katika tendo la ndoa.
• Sio swala la kushiriki tu. • Mnaweza mkawa mnashiriki lakini je
ushirika huo unamridhisha kila mmoja wenu? • Mmoja anapokuwa anapunjika
kila siku anakula lakini hashibi, inafungua mlango wa kumtafuta
mshibishaji mwingine ili aweze kumshibisha. • Tatizo hili ni kubwa sana
hasa kwa siku za leo. • Wanaume wengi ni wavivu na wenye ubinafsi. •
Wanalishwa vizuri ila wanajishibisha wenyewe tu na kuwaacha wake zao
wakiishi kwa njaa ya muda mrefu na matokeo yake michepuko imekuwa
ikiongezeka kila iitwapo leo.
10. Kufanya kazi pamoja mwanamke na mwaname asiye mwenzi wako kwa muda mrefu.
• Sumaku na bati vikikaa karibu mwishowe vitanasa. • Mwanamke na
mwanaume wanaofanya kazi pamoja kwa muda mrefu wakiwa katika mazingira
ya private huishia katika kutamaniana. • Kazi za kusafiri kwa pamoja
mwanamke na mwanaume na kukaa hotel moja kikazi wakiwa wawili tu huweza
kuongeza kazi ya ziada ambayo ni sumu kwa ndoa zao. • Kwenda kusoma
pamoja kozi za nje kati ya wawili hao, wanaweza kuvumila sikuchache za
kwanza na baada ya hapo huweza kujikuta wakiwa katika ukurasa mwingine. •
Kwenda safari mbali za kikazi pamoja umakini usipozingatiwa ni majanga.
• Kufanya vikao katika vyumba vya hotel mwanamke na mwanaume. •
Kujifungia kufanya counselling au maombezi mwanamke na mwanaume wawili
tu chumbani ni majanga. • Kujifungia chumbani mwanaume na mwanamke
wawili tu kusoma na kubukua kwajili ya mtihani ni majanga