VIGEZO 10 VYA KUMPATA MUME/MKE /MCHUMBA MWENYE MAPENZI YA KWELI
Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa
masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha
kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.
Watalaam hao wanataja
safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo
inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na
uhusiano na dazeni ya wapenzi.
Wanasema msichana/mvulana
anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono,
hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu
ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.
Kwa mantiki hiyo, bila
upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli
hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye
huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya
kupata penzi la kweli.
Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa
kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha
wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.
Ukweli ni kwamba mtu
aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke
asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza
katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia
wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.
Mwanamnke mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Ramla aliwahi kuniomba ushauri, akasema
amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo
lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari
ameshafanya mapenzi na wanaume hao.
Na leo my best friend na mdau wangu mkubwa wa Blog hii Rayha ametaka
kujua vigezo gani vya kuzingatia ili kumpata mume/mpenzi borana mwenye
mapenzi ya kweli na ya dhati , hii ameiandika kwenye ukurasa wake wa
facebook.
Nia ya swali lake ilikuwa ni
kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi?
Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa
na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo
huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.
Binafsi
nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika
mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa
kitoto wa pata potea.
Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo
vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye
mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na
mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko
kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.
Ifuatavyo
ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata
mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la
kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa
kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.
KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.
Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa
aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua
wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa
mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.
PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.
TATU- Anza
kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu
macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje
na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako
hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.
NNE -
Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa
suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi
unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya
kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na
makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.
Katika uchunguzi huu
mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha
huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka
alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza
amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila
kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.
TANO - Ajipe muda wa
kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha
aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi
mwanaume huyo alivyopata au kukosa.
Ikibainika mwanaume
aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa,
basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia
kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.
Lakini angalizo
kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika
kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni
mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni
vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.
SITA
- Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya
kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao.
Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na
wanapokwenda.
Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime
umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda
kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri
usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na
mara zote wasaidiane kwa ukaribu.
SABA - Ni vema ndugu
wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni
budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya
wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa
wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha
kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono
uhusiano wa wanaotaka kuoana
NANE - Hatua hii ni ya kuweza
kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia
kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na
kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili
basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.
TISA - Kutimizwa
kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua
muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja
moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.
KUMI -
Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na
changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana
ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana
udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko
hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya
mwanandoa asivutiwe na mwenzake.
Mwisho ni kwamba kanuni hizi
huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara
mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na
maradhi
The Casinos in 2021 - Lucky Club Live
ReplyDeleteHow many casinos in the UK have slots and table games? — In many cases, there is an luckyclub.live abundance of online casinos for you. However, there are also